Muimbaji huyo alikuwa akiongea kwenye kipindi cha 360 cha Clouds TV leo asubuhi ambapo aliulizwa ni msanii gani wa nje ya Afrika anayependa kufanya naye kazi.
Diamond alidai kuwa tayari msanii anayemkubali zaidi nchini Marekani ameshafanya naye kazi japo hakupenda kumtaja tena.
Aliombwa amtaje msanii mwingine tofauti na huyo na kusema wasanii watano anaowapenda zaidi nchini Marekani ni Nicki Minaj, Chris Brown na Usher Raymond na kwamba mmoja kati ya hao tayari ameshafanya naye ngoma!
So ubashiri wetu ni Usher!
0 comments:
Post a Comment