Spika wa bunge alikimbia Bunge…

susanSpika wa Bunge la County ya Nakuru Kenya, Susan Kihika amekimbia kutoka Bungeni baada ya vurugu kuibuka huku Wabunge wakimshutumu kwa uongozi mbovu.
Shughuli za Bunge zilianza kama kawaida na baadaye hali ilibadilika ghafla, Spika huyo akaanza kushambuliwa kwa  matusi huku Wabunge wakosigelea meza yake kutaka kumpiga.
Hali hiyo ilitokana na Spika huyo kusoma barua moja kutoka Mahakamani ambayo iliibua mzozo na kufanya kundi moja la Wabunge kuanza kumshambulia na kutaka kumpiga hali iliyomfanya akimbie nje akiongozana na walinzi wa Bunge na kupanda kwenye gaei yake haraka na kukimbizwa kutoka eneo la Bunge hilo huku Wabunge wakilikimbiza gari hilo.
Mzozo huo unatokana na ishu ya vikundi viwili kuzozana ndani ya Bunge kutokana na amri ya Mahakama kumtangaza Samuel Waithiki kama kiongozi badala ya Maura Njenga.
Wabunge wengine walibaki ndani ya Bunge wakimtaka Spika huyo ajiuzulu.

Share on Google Plus

About ahmed

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment