Studio mpya za Azam TV zawa gumzo zafananishwa na CNN, Aljazeera, BBC, ujenzi umegharimu bilioni 56 – Tido Mhando

Azam-1Uzinduzi wa studio mpya za kisasa za Azam TV zilizoko eneo la Tabata Relini, jijini Dar es salaam unafanyika leo.
TIDO
Naibu Mtendaji Mkuu wa Azam Media Limited, Tido Mhando ambao ndio wamiliki wa Azam TV, aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa studio hizo zimegharimu zaidi ya bilioni 56.
Azam-1
Studio mpya za Azam TV
“Ni studio ambazo labda unaweza ukazifananisha na kampuni kubwa kama CNN, Aljazeera, BBC, na kwakuwa za kwetu ni mpya zinaweza kuwa na ubora kuliko hizo,” alisema Tido.
Azam-2
Tido aliendelea,
“Azam TV imeanza kufanya shughuli zake kwa zaidi ya mwaka sasa, lakini tumekuwa tukiboresha mambo kadha wa kadha kuelekea siku ya kesho (leo) ambayo tunaweza tukasema ndiyo mwanzo rasmi wa Azam Tv.”
Rais Kikwete anatarajiwa kuzindua studio hizo leo March 6.
Picha: Biz Zubeiry
Share on Google Plus

About ahmed

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment