Chris Brown apigwa chini na girlfriend wake baada ya kuenea kwa taarifa kuwa ana mtoto na msichana mwingine
TMZ iliripoti kuwa Chris Brown alimzalisha model wa zamani aitwaye Nia, ambaye hata Karrueche alikuwa anamfahamu na waliwahi kula bata pamoja lakini hakujua kama amezaa na Breezy.
Karrueche ambaye hana muda mrefu sana toka arudiane na Breezy waliyeachana miezi kadhaa iliyopita, ameshindwa kuvumilia na kuutangazia ulimwengu uamuzi alioamua kuuchukua baada ya kufahamu uwepo wa kiumbe chenye damu ya boyfriend wake.
Kupitia Twitter Karrueche ameandika:
“Listen. One can only take so much. The best of luck to Chris and his family. No baby drama for me.”
0 comments:
Post a Comment