Rama Dee kuvunja ukimya kwa kuachia ‘Usihofie Wachaga’, aeleza kilichomweka busy

Muimbaji wa muziki wa R&B aliyehamishia makazi yake nchini Australia, Rama Dee, anatarajia kuvunja ukimya wake wa zaidi ya mwaka mmoja kwa kuachia wimbo mpya uitwao ‘Usihofie Wachaga’
20150305002115 (1)
Rama Dee ameiambia Bongo5 kuwa wimbo huo utatoka wiki mbili kuanzia sasa na ameurekodia kwenye studio za Home Town chini ya producer Elly Da Bway aliyetengeneza wimbo wake ‘Kama Huwezi’ aliomshirikisha Lady Jaydee.
Akizungumzia maana ya wimbo wake huo mpya, Rama amedai kuwa unahusiana na ile imani iliyojengeka kwa baadhi ya wanaume wa Tanzania kuwa wanawake wa kichaga wanapenda pesa tu na hawana mapenzi.
“Katika makabila makubwa hapo Tanzania yasemwayo vibaya ni wachaga so nipo na sababu ya kusema usihofie kama upendo upo upo tu kwani mchaga hapendi,?” amehoji muimbaji huyo.
“Nimetaja mambo mengi ila naona wachaga na makabila mengine ni muda wa kupendana tu sio kubaguana tabia ni ya mtu binafsi hata huku mbele kuna watu wenye tabia mbaya so sio issue ya kabila ni issue ya upendo,” ameongeza.
20150305002115
Kwa upande mwingine Rama Dee amedai kuwa masomo na kupata mtoto wa pili wa kiume aitwaye Cedric ni sababu zilizomfanya awe kimya.
“Niliona niongeze elimu zaidi maana haya mambo ya muziki yapo na mashabiki wapo. Halafu kingine niliongeza familia so sikuweza kugawa muda kwa sehemu zote,” amesema.
“Kwa sasa nitakuwepo kwenye masikio ya watu bila shaka. Watu walihitaji kazi zangu sina budi kuzifanya kwa uweledi.”
Share on Google Plus

About ahmed

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment