Sina bifu na Van Gaal, asema Ryan Giggs

 
Rayan Giggs na mkufunzi Louis van Gaal 

Naibu mkufunzi katika timu ya Manchester United Ryan Giggs amepinga madai ya mkwaruzano kati yake na mkufunzi wa kilabu hiyo Louis Van Gaal.

Uvumi wa wasiwasi kati ya makocha hao wawili ulizuka baada ya Giggs kukataa kusherehekea bao la ushindi la Ashley Young siku ya jumatano.

Aliyekuwa mchezaji mwenza katika kilabu hiyo Paul Scholes alisema kwamba Giggs amechoka kuwa mkufunzi chini Ya Louis Van Gaal kwa miaka mitatu ijayo.

Lakini Giggs amesema kuwa wawili hao wana ushirikiano mzuri kati yao na kwamba anafurahia kazi yake chini ya mkufunzi Van Gaal.

Share on Google Plus

About ahmed

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment