Shirikisho la Soka nchini Uingereza
FA limewapiga marufuku wachezaji Jonny Evans wa Manchester United na
Papiss Cisse wa Newcastle kutocheza mechi saba kwa kutemeana mate.
Evans
mwenye umri wa miaka 27 alikuwa amekana mashtaka ya kumtemea mate Cisse
katika mechi dhidi ya Manchester ambapo kilabu hiyo ya Old Trafford
iliibuka mshindi kwa 1-0.Bwana Evans alipinga madai hayo lakini yakabainishwa,ilisema taarifa ya FA.
Cisse mwenye umri wa miaka 29 alikubali mashtaka aliyowekewa na sasa amepigwa marufuku kwa mechi nane kwa kuwa tayari alikuwa amehudumia marufuku msimu huu.
0 comments:
Post a Comment