Wachezaji watano wa kilabu ya Kano
Pillars nchini Nigeria walipigwa risasi na wapiganaji katika shambulizi
lillolenga msafara wa kilabu hiyo wakati wachezaji hao walipokuwa
wakielekea Owerri katika mechi ya ufunguzi wa Ligi kuu nchini Nigeria.
Wapiganaji hao pia walichukua simu pamoja na vitu vyengine muhimu vya wachezaji hao.Mechi iliokuwa ichezwe siku ya jumamosi kati ya timu hiyo na ile ya Heartland imeahirishwa mara moja.
Kilabu hiyo ya Kano Piilars ilikuwa ndani ya basi lililowabeba wachezaji 25,ikiwemo wachezaji 18,wakati wa tukio hilo lililotokea mwendo wa saa saba na robo saa za Nigeria.
0 comments:
Post a Comment