Mshambuliaji wa kilabu ya Swansea
Bafetimbi Gomis alianguka na kuzirai uwanjani, ikiwa ni kisa cha hivi
karibuni cha mchezaji huyo ambaye amekuwa akikabiliwa na tatizo hilo
mara kwa mara.
Swansea ilikuwa ikimenyana na kilabu ya Totenham
Hospurs wakati wa tukio hilo na kusababisha mchezo kusimamishwa kwa
dakika tano ili madaktari kumuhudumia mchezaji huyo.Mechi hiyo ilikamilika ikiwa Totenham imeibuka kidedea kwa mabao 3-2
Raia
huyo wa Ufaransa amekabiliwa na visa kama hivyo ikiwemo visa vitatu
alipokuwa akiichezea kilabu ya Lyon mnamo mwaka 2009 na chengine wakati
alipokuwa katika kambi ya mazoezi na, wasiwasi uliwazonga wachezaji
wenzake katikati ya uwanja alipokuwa akipokea matibabu.
Baadaye mchezaji huyo alituma ujumbe wake katika mtandao wa tweeter akiwashukuru mashabiki kwa kuonyesha umoja wao naye na kuelezea kwamba hali yake ya afya imesababishwa na wasiwasi alionao kuhusu afya ya babaake nchini Ufaransa.
Aliandika:''Ningependa kuwahakikishia kuhusu afya yangu.
Pengine tukio hilo linaonyesha kwamba afya yangu imezorota ikilinganishwa na nilivyo sasa.
Tatizo hili linasababishwa na uchovu unaosababishwa na wasiwasi nilionao kuhusu afya ya babaangu ambapo mimi hulazimika kusafiri kwa mda mrefu kwenda na kutoka Ufaransa kila mara''.
0 comments:
Post a Comment