Kuna tetesi za miezi kadhaa sasa mtaani (ambazo sisi binafsi
hatujaweza kuzithibitisha) kuwa Meninah alitoa mimba aliyopewa na
Diamond Platnumz.
Wawili hao waliwahi kudaiwa kuwa na uhusiano lakini wote walikanusha.
Mtangazaji mahiri wa masuala ya udaku nchini, Soudy Brown kupitia You
Heard ya Clouds FM amejaribu kumchimba Meninah kuhusiana na tetesi hizo
ambazo zinaongeza kuwa Diamond alimpiga chini baada ya kiumbe chake
kukatishwa.
Hata hivyo huenda jibu alilopata mtangazaji huyo hakuwa amelitegemea.
“Kwani (Diamond) sio rijali,” alihoji mrembo huyo. “Yeye hafai kumbebesha mwanamke mimba,” alisisitiza Meninah huku akicheka.
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment