MWANAFUNZI ALIYEONGOZA MATOKEO KIDATO CHA NNE 2014

 
Mwanafunzi bora wa mtihani wa Kidato cha Nne mwaka 2014, Nyakaho Marungu (16), amesema mazingira mazuri ya kusomea na msaada alioupata kutoka kwa wazazi wake ndiyo uliofanisha afike hapo.

Marungu mkazi wa Kitunda alitoa kauli hiyo jana jijini Dar e Salaam wakati akizungumza nasi Jumapili na kueleza kuwa,ufaulu huo pia ulitokana na umakini wake katika masomo.

Mwanafunzi huo ambaye alikuwa anasoma katika Shule ya Sekondari ya Baobab iliyopo Bagamoyo Mkoani Pwani, amekuwa wa kwanza kati ya wanafunzi 196,805 waliofanya mtihani huo mwaka jana baada ya kuibuka na pointi  5.1.

"Nilitarajia kufanya vizuri lakini sikujua kama nitakuwa mwanafunzi bora wa mwaka 2014 nchi zima,” alisema.

Nyakaho ambaye wakati wote alionyesha uso wa furaha akiwa nyumbani kwa wazazi wake, alisema anawashukuru wazazi wake, walimu na mazingira mazuri ya shuleni yaliyomfikisha hapo.

“Jitihada binafsi, kujituma kusoma kwa bidii hasa wakati wa usiku, pia uwepo wa vifaa vya kutosha shuleni pamoja na vitabu umesaidia sana” alisema na kuongeza:.

“Shule ina vifaa vya kutosha ikiwa ni pamoja na maabara nzuri ya kisasa na kuongeza pia anapendelea kusomea masomo ya sayansi,” alisema.

Alisema, wakati wote akiwa shuleni alitumia muda mwingi kujisomea kwa kuwa aliamini mafanikio hayapatikani bila kujituma.

Mama wa mtoto huyo, Selestina Maro, alisema Nyakaho ni mtoto wake wa pili na kwamba mafaniko yake yametokana na jitihada zake binafsi.

"Darasa la saba alifaulu kwenda shule ya sekondari ya Jangwani lakini tuliamua kumpeleka St. Thereza iliyopo Arusha ambapo huko alisoma mwaka mmoja, shule ya Baobab alianza kidato cha pili hadi akamaliza, " alisema na kuongeza:

"Ushauri wangu kwa wazazi na walezi wafuatilieni watoto wenu wanapotoka likizo au wanaporudi kutoka shule siyo kuangalia televisheni, hakikisheni wanakazania masomo," alisema.




Mwanafunzi aliyeongoza kwa kufanya vizuri katika mtihani wa kidato cha nne kitaifa mwaka jana, Nyakaho Marungu akipongezwa na mama yake Celestina Maro, nyumbani kwao Kitunda Dar es Salaam jana, muda mfupi baada ya Baraza la Mitihani la Taifa (Necta), kutangaza matokeo ya mtihani huo. Picha na Goodluck Eliona


Share on Google Plus

About ahmed

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment