Ukiwa kiongozi kwenye nafasi yoyote
lawama huwezi kuzikwepa, tumesikia wananchi wakilalamikia matumizi
mabaya ya fedha yanayofanywa na viongozi, hizi lawama haziko bongo peke
yake kuna hii kwenye headlines za India.
Waziri mkuu wa India Narendra Modi kununua suti ya gharama ambayo aliivaa kwenye mapokezi ya Rais Barack Obama alipotembelea
India mwezi January nayo imekuwa ishu! headlines za vyombo vya habari
India zimeandika kuhusu wananchi kulalamika gharama za suti hiyo, eti
wanadai gharama haziendani na maisha ya wananchi wanavyoishi.
Suti ya Waziri huyo iligharimu zaidi ya
dola 16,000 (kama milioni 30 za kibongo), wananchi wanadai ametumia pesa
nyingi kushona suti huku akishindwa kutekeleza ahadi ya kuboresha
maisha yao.
Moja ya kitu kinachoifanya suti hii kuwa
na gharama kubwa ni upekee wake, ina mistari midogo midogo ambayo
ukiiangalia kwa ukaribu ni maandishi yaliyoandikwa jina la Waziri Mkuu
huyo.
Waziri Mkuu Ghandi ametangaza kuipiga mnada suti hiyo ili iuzwe na pesa itakayopatikana ichangie masuala mengine ya maendeleo kwa watu.
Makamu wa Rais wa India Rahul Ghandi naye ni kama anaunga mkono kinachosemwa na wananchi hao.
0 comments:
Post a Comment