Matonya: Tundaman ndo mwizi wa pesa zangu benki

Matonya na Tundaman wameingia kwenye vita vya maneno. Ugomvi huo umeanza baada ya Tundaman kudai kuwa alimtungia wimbo Matonya kwenye album yake ya Vailet.

Akiongea kwenye 255 ya XXL kupitia Clouds FM jana, Matonya alikanusha taarifa hiyo na kwamba Tundaman hana uwezo wa kumtungia wimbo kwakuwa uimbaji wao upo tofauti kabisa.
“Nilikuwa naenda na Tunda sehemu zote ninazoenda, studio sehemu ambazo kwa raha zangu na nikiwa na shida zangu tunaenda wote, anafika nyumbani Tanga ni mwanafamilia,” alisema. “I swear to God, mama anampenda sana. Ndo alikuwa kijana wangu wa karibu, material yangu nilikuwa nampatia yeye. Sijaja hapa kutokana sikupata nafasi ya kuongea. Material yangu anayatumia, nina kazi yangu ninamuuliza ‘ndugu yangu hapa nafanya nini? Mdogo wangu tufanye hivi namsikiliza’, lakini hakuna mtu ambaye anaweza kuniandikia mimi nyimbo,” alisisitiza.
“Mimi nina njia zangu tofauti na mimi ni mtoto wa kitanga, Tunda man kwenye key zangu hafiki, aje leo hapa afiki kwenye key. Mimi alishachukua kazi zangu na akaniibia benki, akachukua pesa zangu. Alikuwa ana serial namba zangu, alichukua hela yangu benki. I swear to God alichukua pesa zangu. Nilimpa kadi yangu aende akatoe hela aliniambia nilikuwa na shida nikampa kadi yangu ya benki. Mungu nisaidie anakuja ananiongelea vibaya why? Akachukua mzigo anaotaka. Mimi nachopenda kusema Tunda ni mdogo wangu na sitaki ugomvi na mtu. Hii ni dunia mimi najua dunia tunapita wote tutakufa mimi naomba Tunda akimaliza utoto wake ajue mimi ni kaka yake.”
Kwa upande wake Tundaman amekanusha tuhuma hizo na kudai ukweli umemuuma Matonya.
“Ujue ukweli siku zote humweka mtu huru,” amesema. “Mimi binafsi sina ugomvi na Matonya sema nimesema ukweli kuhusu hali iliyopo. Siwezi kumuibia Matonya nina miaka kama mitano hivi sijakaa naye chini. Yeye baada ya kusikia mimi nimeweka ukweli kusuhu album ndo yamekuwa hayo. Hilo suala la kuiba benki hela yake ni uongo. Mimi na masuala ya benki tunahusiana vitu na sina uwezo wa kufanya hivyo. Sio kweli au lini amenituma nikamtolee hela? Huyu ana create tu anatakiwa akubali huyu jamaa alikuwa ananitungia ndo solution, sasa yeye ana create uongo ati nilimwibia miaka sita alikuwa wapi asiseme!”
Share on Google Plus

About ahmed

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment