KAJALA KUZAA MTOTO MWINGINE HUKU MUMEWE BADO YUKO JELA
Kajala Masanja akiwa na mwanaye Paula.
Mwanadada anayeendesha maisha yake kwa kuuza sura kwenye filamu za Kibongo, Kajala Masanja amefunguka kuwa ni muda muafaka wa kufanya mishemishe za kumtafuta mtoto mwingine kwani yule wa kwanza, Paula ameshakua.
Akizungumzia mipango yake kwa sasa hasa kwenye suala la kuongeza mtoto, Kajala alisema umri unazidi kuyoyoma na Paula anazidi kuwa mkubwa hivyo ni vyema akamtafutia mdogo wake fasta kabla ya kuamua kutulia.
“Kwa kweli nahitaji kumpata mdogo wake Paula haraka, umri unazidi kusonga mbele, siyo nakuja kuzaa tena Paula kishakuwa mdada mkubwa, itakuwa aibu,” alisema Kajala.
0 comments:
Post a Comment