AZAM ITAWEZA KUIVUTA YANGA KILELENII?

 
Mabingwa wa Tanzania Bara, Azam itacheza na Mtibwa Sugar Jumatano hii katika jitihada za kuiondoa kileleni mwa ligi, klabu ya Yanga.
 
Azam, baada ya kutoka sare ya 2-2 na Polisi Morogoro hivi karibuni, inahitaji pointi tatu muhimu ili kufikisha pointi 25, kuwa kileleni sawa na Yanga.

Yanga ilifanikiwa kuwa kileleni mwa ligi kuu ya timu 14 baada ya kuifunga Mtibwa Sugar 2-0 katika uwanja wa Taifa, Dar es Salaam juma lililopita.

Hata hivyo, Azam, ambao ni wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika, wasitegemee ushindi mwepesi kwani wapinzani wao, Mtibwa Sukari wamesema hawapo tayari kupoteza mechi mbili kwa mfululizo katika jitihada zao za kutafuta ubingwa kwa mara ya kwanza.

Endapo watafanikiwa kuwafunga Azam, Mtibwa ikiwa chini ya kocha Mecky Mexime, nahodha wa zamani wa timu ya taifa (Taifa Stars),itafikisha pointi 21. Mtibwa ilishawahi kuwa mabingwa wa Tanzania Bara mara mbili mfululizo, mwaka 1999-2000 huku Azam ikiwa ni mabingwa mara moja katika msimu uliopita
Share on Google Plus

About ahmed

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment