KWELI kifo hakina huruma jamani! Mshiriki wa Miss Tanzania 2013 akitokea Miss Ilala, Martha Gewe, mkazi wa Tabata Segerea, Dar amefariki dunia baada ya kuugua ghafla, Ijumaa Wikienda linakupa zaidi.
Marafiki wa aliyekuwa mshiriki wa Miss Tanzania 2013 akitokea Miss Ilala, Martha Gewe wakiwa na huzuni.
Martha
amekutwa na mauti katika Hospitali ya Mkoa wa Ilala, Amana jijini Dar
es Salaam, Ijumaa iliyopita ambako alikimbizwa baada ya kuugua na
madaktari walibaini kwamba, malaria ilipanda kichwani.AFYA YAKE SIKU ZA NYUMA
Habari zaidi zinasema kuwa mrembo huyo hakuwa akisumbuliwa na ugonjwa wowote huko nyuma na alionekana mwenye afya njema huku mipango yake ikiwa imelenga jinsi atakavyoisherehekea Sikukuu ya Krismasi.
“Lakini Jumatano iliyopita alianza kuumwa, alisema anahisi homa ambayo baadaye ikabainika ni malaria.
Mwili wa marehemu Martha Gewe ukiwa kwenye jeneza.
“Tulimpeleka Amana, akalazwa kwa siku tatu tu, leo (Ijumaa) akafariki dunia. Madaktari wamesema ile malaria kukimbilia kichwani ndiyo tatizo,” alisema ndugu mmoja wa marehemu huyo kwa sharti la kutochorwa jina gazetini kwa kuwa siyo msemaji wa familia ya mzee Gewe.
WALICHOSEMA MADAKTARI
Ijumaa Wikienda lilifanikiwa kuzungumza na madaktari wawili wa Hospitali ya Amana jijini Dar kuhusu ugonjwa wa malaria kupanda kichwani.
“Mpaka sasa bado malaria ni tishio, inaua watu wengi sana. Kwa malaria kupanda kichwani ni hatari zaidi kwani mgonjwa anaweza kupoteza maisha ndani ya muda mfupi sana.Ijumaa Wikienda lilifanikiwa kuzungumza na madaktari wawili wa Hospitali ya Amana jijini Dar kuhusu ugonjwa wa malaria kupanda kichwani.
“Kikubwa watu wazingatie kuwa mbali na mazingira hatarishi kwa ugonjwa huo na wajichunge kuumwa na mbu ambao ndiyo wana-oeneza ugonjwa huo,” alisema daktari mmoja.
MAMISI WENZAKE NI MACHOZI
Kufuatia taarifa za kifo hicho, mamisi wenzake walipigwa na mshangao, wengine wakiuliza nini kilimpata mwenzao huyo!
“Kwa kweli nilipopata taarifa za kifo cha Martha sikuamini mara moja kwa vile sijawahi kusikia akiumwa au hata kwamba alilazwa kwa muda mrefu.Kufuatia taarifa za kifo hicho, mamisi wenzake walipigwa na mshangao, wengine wakiuliza nini kilimpata mwenzao huyo!
“Kifo chake kimeniumiza sana, sijui hata nisemeje jamani, kweli kifo hakina huruma,” alisema Miss Ilala 2013, Dorice Mollel huku akilia.
Mrembo mmoja ambaye hakutaja jina lake alisikika akisema: “Yaani Happiness (Watimanywa) yuko Uingereza kusaka taji mwenzake anapoteza maisha ghafla hapa nyumbani Tanzania! Inauma sana kwa kweli.”
Warembo wengine walioshiriki msiba wa Martha nyumbani kwao, Tabata, Dar walishindwa kujizuia na kujikuta wakibubujikwa machozi muda wote kiasi cha kushindwa kuongea na mwandishi wa gazeti hili.
HISTORIA YA MARTHA KATIKA UMISI
Mwaka jana, Martha alishiriki shindano la kumsaka Redd’s Miss Ukonga lililofanyika katika Ukumbi wa Wenge Garden, Ukonga Mombasa jijini Dar.
Katika kinyang’anyiro hicho, Martha aliibuka kidedea kwa kuvalishwa taji hivyo kupata tiketi ya kwenda kushiriki Miss Ilala 2013 kwenye Ukumbi wa Golden Jubilee Tower, Dar ambapo mshindi alikuwa Dorice.
Marehemu alipata nafasi ya kuvuka Miss Ilala na kushiriki Redd’s Miss Tanzania 2013 chini ya Hashim Lundenga ‘Anko’ na kufanikiwa kuwa miongoni mwa Kumi Bora huku Happiness Watimanywa akiibuka mshindi.
Watimanywa usiku wa kuamkia leo, kule jijini London, Uingereza alifurukuta kugombea Taji la Miss World!Marehemu alipata nafasi ya kuvuka Miss Ilala na kushiriki Redd’s Miss Tanzania 2013 chini ya Hashim Lundenga ‘Anko’ na kufanikiwa kuwa miongoni mwa Kumi Bora huku Happiness Watimanywa akiibuka mshindi.
MAZISHI YA MARTHA
0 comments:
Post a Comment