NI SHEEDA! MUIGIZAJI WA FILAMU SLIM ADAIWA KUGOMA KUREJESHA GARI


NI sheeda! Muigizaji wa filamu za Kibongo, Salim Omary ‘Slim’ amejikuta akiwekwa nguvuni katika Kituo cha Polisi cha Makangarawe, Yombo-Buza, jijini Dar akidaiwa kugoma kurejesha gari aina ya Land Lover Discovery walilopewa zawadi siku ya ndoa.
Muigizaji wa filamu za Kibongo, Salim Omary ‘Slim’.
Gari hilo walipewa na wakwe zake alipofunga ndoa na binti yao aitwaye Asia Morgan, mwaka jana lakini ilipofika Mei mwaka huu (takriban miezi tisa tu ndani ya ndoa), wawili hao walitengana na kusababisha wakwe hao wageuke mbogo kudai chao kwa maelezo kwamba walitoa zawadi hiyo kwa binti yao hivyo kwa kuwa wametengana, wanataka chao.
Kwa mujibu wa chanzo chetu, Asia alifikia uamuzi wa kwenda kuishi nyumbani kwao Tegeta, jijini Dar baada ya kushindwa kuvumilia tabia ya wivu wa kupindukia aliyokuwa nayo Slim.
“Baada ya kutengana wazazi wa msichana huyo walimwambia Slim awakabidhi gari moja kwa kuwa anayo mawili na kama anataka Discovery (Land Lover) wamuachie lakini wapate moja kwa ajili ya binti yao kuendea chuo,” kilisema chanzo.
Salim Omary ‘Slim’ akiwa na aliyekuwa mke wake.
Akizungumza kwa jazba, mama mzazi wa Asia alisema, walimzawadia gari hilo kwa kuwa wote walikuwa wanapenda tasnia ya filamu hivyo gari hilo lingemsaidia yeye na mume wake katika shughuli zao.
“Kinachouma ni kwamba tusingefikishana hapa lakini tulishamuomba sana Slim kurudisha gari hilo au ampe mwanetu gari lingine abaki na hilo kama analipenda lakini alikataa na mbaya zaidi ana kila kitu, kuanzia ufunguo na kadi ya gari kitu ambacho hatendi haki kwa mtoto wetu,” alisema mzazi huyo.
kizidi kutema cheche mbele ya kinasa sauti cha Ijumaa, mzazi huyo alisema licha ya Slim kwenda Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata) kushtaki ili arudiane na binti yao, haitawezekana.
“Nashindwa kuelewa kabisa jambo hili nilijitahidi sana kulivumilia lakini nimeona imeshindikana kabisa hivyo tuliamua kwenda nyumbani na kumchukua kumfikisha kituoni hapa maana sisi tulimfanya kama mtoto wetu lakini yeye amekuwa mkaidi,” alisema mama huyo.
Salim Omary ‘Slim’akiwa katika kituo cha polisi Makangarawe, Yombo-Buza.
Mwandishi wetu alimfuata Slim kituoni hapo na kuzungumza naye kuhusiana na sakata hilo ambapo alisema anachofahamu yeye ni kwamba zawadi inapotolewa kwenye harusi na wazazi inakuwa ni ya mke na mume lakini anawashangaa wazazi hao kuidai ikiwa hata mkewe hajampa talaka.
“Nashindwa kuelewa kabisa kwa sababu wazazi wa mke wangu walitoa gari lile kama zawadi sasa sielewi kwa nini walidai tena wakati mke wangu sijamuacha, suala hili lipo Bakwata.
“Isitoshe, gari hilo nimelitengeneza sana mpaka kufikia lilivyo sasa kwani bado lipo gereji, lakini kwa kuwa wameamua kunidai, baada ya miezi mitatu nitakuwa nimewapa gari lao,” alisema Slim.
Share on Google Plus

About ahmed

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment