BANZA AANIKA SIRI YA SHAVU DODO LAKE
Wenye kumbu-kumbu wanafahamu jinsi mwanamuziki wa Bendi ya Extra Bongo, Ramadhan Masanja ‘Banza’ alivyokuwa amekonda lakini sasa anaonekana kuwa na shavu dodo kiasi cha baadhi ya watu kuwa na hisia tofauti ila mwenyewe anaanika siri ya kufutuka ghafla.
Akipiga stori na Ijumaa, Banza alisema awali alikuwa hajali suala la kula vizuri, badala yake alikuwa akiendekeza pombe kiasi cha kumfanya akose afya nzuri.
“Ukweli siri ya kuwa na afya njema sasa ni kwamba nakula vizuri na kwa wakati pia nimepunguza kunywa pombe kwani siku zilizopita nilikuwa nakunywa sana mpaka nikasimamishwa kazi lakini sasa nimebadilika,” alisema Banza
0 comments:
Post a Comment