Mkuu wa shule ya sekondari ya Ifunda akizungumza na wanafunzi hao hivi karibuni.
Wanafunzi wa shule ya sekondari ya Ufundi Ifunda.
Uongozi wa shule ya sekondari ya Ufundi Ifunda mkoani Iringa
imewaita wanafunzi 28 kufika shuleni hapo octoba 2 ikiwa ni baada ya
shule hiyo kufungwa kwa muda usiojulikana kutokana na wanafunzi hao
kufanya vurugu kubwa hivi karibuni.
Hatua ya uongozi wa shule hiyo kuwaita wanafunzi hao imekuja zikiwa
ni zaidi ya siku 4 kupita toka shule hiyo kufungwa kufuatia vurugu
kubwa shuleni hapo na kusababisha hasara kubwa ya mali za shule
hiyo.
Makamu mkuu wa shule hiyo Ernest Sakafu ameyasema hayo Leo wakati akizungumza na mtandao wa matukio daima ofisini kwake.
Amewataja wanafunzi wanaotakuwa kufika shuleni hapo kuwa ni steven
Nyiriri, petro Kalolo, Iddi Shaban, John Zephania, Edwin Rwegoshora,
Adinan Mrisho Mtiti, Izengo Dotto, Gaspar Manyagi, Shemson Amoni ,Halid
Omari, Said Sambo, Paschal lusukanija , Fred Kidava na Eliji Nguvila
Wengine ni Stambuli Daluweshi, Jackson Mlowe,Sidi Kayombo,Yusuph
Makale , Joseph Antony ,Allan Laurent, Rose Kayombo, Enoce John, Rashid
Kandoro, Abdul Zumo, Petro Silwimba, Joyce Nestory , Michael Kimario na
Athuman Ahamad.
Alisema kuwa kwa sasa shule hiyo imefungwa kutokana na vurugu hizo hivyo shule hiyo itafunguliwa wakati wowote kuanzia sasa.
0 comments:
Post a Comment