Rais wa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Tiba na Teknolojia IMTU (IMTUSO), Meekson Mambo.
Rais wa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Tiba na Teknolojia IMTU (IMTUSO), (katikati), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari
Dar es Salaam leo, wakati akitoa taarifa kwa umma kufuatia maagizo ya
Tume ya vyuo vikuu Tanzania (TCU) dhidi ya chuo cha IMTU. Kulia ni Naibu
Naibu Waziri wa Mikopo na Ruzuku wa IMTU, Benson Lukwambe na Makamu wa
Rais, Walter Nnko.
Dotto Mwaibale
WANAFUNZI wa Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Tiba na Teknolojia
IMTU wameiomba Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) kuunda tume maalumu
itakayoshirikisha uongozi wa wanafunzi kufuatia utekelezaji wa maagizo
waliyokiwekea chuo hicho ili kukamilisha kwa muda uliopangwa.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo Rais wa
Serikali ya wanafunzi wa chuo hicho,IMTU (IMTUSO), Meekson Mambo alisema
wanafunzi wa chuo hicho wana wasiwasi kuhusiana na muda wa miezi mitatu
uliotolewa na TCU kuhakikisha chuo cha IMTU kimekamilisha masharti
yote waliyopewa vinginevyo kitafungwa.
"Matatizo ya chuo hicho ni ya muda mrefu hivyo kukiwa na kamati
maalumu itasaidia kushughulikia suala hilo haraka na kulitafutia
ufumbuzi badala ya kukifunga chuo hicho ambako kutaleta athari kubwa
katika masomo kwa wanafunzi" alisema Mambo.
Mambo alisema TCU iunde kamati ya muda itakayoshirikiana na uongozi
wa chuo uliopo sasa pamoja na uongozi wa wanafunzi waweze kusimamia na
kuhakikisha kuwa maagizo ya TCU yanatekelezwa ili kutoa fursa kwa
wanafunzi kuendelea na masomo huku mapungufu ya muda mrefu yaliyopo
yakiendelea kutatuliwa kwani muda huo wa miezi mitatu waliopewa ni
mdogo.
Aliongeza kuwa endapo uongozi wa chuo utashindwa kutekeleza maagizo
ya TCU hawaungi mkono hoja ya kufunga chuo badala yake kiwekwe chini ya
serikali au chuo kikuu kingine ambacho kina kitakuwa na uwezo wa
kusimamia mfano Chuo Kikuu cha Dar es Salaa ambacho hakina kitivo cha
afya.
Makamu wa Rais wa Serikali ya chuo hicho, WalterNnko alisema
kukifunga chuo hicho kutawaathiri wanafunzi zaidi ya 1000 waliopo chuoni
hapo.
0 comments:
Post a Comment