Baadhi ya Marais,Wenyeviti na Wakurugenzi wa Makampuni mbalimbali ya nchini Marekani waliokuja nchini kwa lengo la kutizama fursa za uwekezaji.
Afisa wa Ubalozi wa Tanzania nchini Washington DC,Suleiman
Saleh (katikati) akibadilishana mawazo na mkurugenzi mtendaji wa
kampuni ya kufua Umeme ya TANASI ,William Crawford.Ziara hiyo inayo
ratibiwa na Ubalozi wa Tanzania,Washington DC ni ya siku ambapo wageni
hao watatembelea sehemu mbalimbali kujionea fursa za uwekezaji.
Afisa
Ubalozi wa Tanzaini ,washington DC ,Suleiman Saleh akizungumza juu ya
ujio wa wageni hao 11 kutoka Marekani ambao wako nchini kwa ajili ya
kutizama fursa ya uwekezaji.Hii ni mara
ya tatu sasa Viongozi wa Makampuni mbalimbali ya Marekani wanafika
nchini ikiwa ni utekelezaji wa mpango wa Rais Kikwete kutekeleza
Dipromasia ya Uchumi.
Rais wa Kampuni ya Ahmed's Moving Express,Inc ,Ahmed Issa,ambaye pia ni Balozi wa heshima akizungumza na waandishi wa habari katika hotel
ya Mount Meru, jijini Arusha kuhusu ujio wa Marais,Wenyeviti na
Wakurugenzi wa makampuni mbalimbali ya Marekani walioko Tanzania .Issa
tayari ambaye ni ziara yake ya tatu sasa kuja Tanzania tayari ameanza
uwekezaji katika sekta ya Utalii ikiwemo kufungua ofisi ya Utalii
Carfonia Marekani iliyozindiliwa hivi karibuni na Rais JAkaya Kikiwete.
Mtaalamu
wa Ujenzi wa nyumba za makazi ,Nishati Erick Nyaren akizungumza na
waandishi wa habari kuhusu ujio wao Tanzania .Nyaren yuko nchini
kuangalia fursa katika uwekezaji katika sekta ya ujenzi na Miundo mbinu.
Mkurugenzi
mtendaji wa kampuni ya kufua Umeme ya TANASI William Crawford akiwa na
mjukuu wake Colin Machamsoc akizungumza na wanahabari kuhusu ziara yao
ya siku sita nchini Tanzania ikiwemo kutembelea vivutio vya utalii vya
,Manyara,Serengeti na Ngorongoro.Crowford yuko nchini kutizama fursa ya
uwekezaji inayopatikana katika sekta ya Kilimo.
0 comments:
Post a Comment