KWA mara ya kwanza Mbunge wa Kigoma
Kaskazini, Zitto Zuberi Kabwe ameibuka na kuzungumzia uhusiano wake na
mtangazaji wa Clouds FM, Loveness Malinzi ‘Diva’ na kufuta uvumi mzito
uliokuwa ukizagaa kuwa wawili hao ni wapenzi.
Mtangazaji wa Clouds FM, Loveness Malinzi ‘Diva’.
Zitto alifunguka hayo juzi kupitia kipindi cha Mkasi kinachorushwa na
Televesheni ya East Africa ambapo alikanusha kuwa hana uhusiano wowote
wa mapenzi licha ya kudaiwa kutungiwa wimbo na mtangazaji huyo kama
ishara ya penzi lao.“Mh! Kama yeye amenitungia wimbo sijui lakini mimi
sina uhusiano naye wowote wa kimapenzi,” alisema Zitto.Katika mahojiano hayo, mheshimiwa huyo alifungukia skendo nyingine inayomhusisha kutembea na staa wa Bongo Fleva, Mwasiti Almasi na kudai hakuna ukweli wowote juu ya ishu hiyo.
Alisema anaumia zaidi kusikia watu wanavyomhusisha kutembea na Mwasiti kupitia mitandao ya kijamii wakati hakuna ukweli wowote ambapo msanii huyo wanaheshimiana na kufanya naye kazi kwa karibu ili kumsaidia katika harakati zake za muziki.
“Naumia sana kusikia wakinisema na Mwasiti wakati yule ni dada yangu na mbaya zaidi ni mtu ambaye mara kwa mara nimekuwa nikimsaidia katika shughuli zake za muziki, hakuna kitu kingine zaidi ya ukaka na udada,” alisema Zitto.
Aidha, mheshimiwa huyo mbali na kungumzia mikakati yake ya kisiasa katika kipindi hicho, aliweka bayana kuwa ni baba wa mtoto mmoja kwa mkewe aliyemtaja kwa jina moja la Jack, wanamlea mtoto wao vizuri lakini suala la ndoa bado halijatimia.
0 comments:
Post a Comment