WASANII waliokuwa wakipigania cheo cha urais wa Manzese, Hamad Ally ‘Madee’, na Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’, hatimaye wamemaliza tofauti zao baada ya kudumu kwenye bifu kwa muda mrefu.
Mkali wa Bongo fleva,Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’.
Ishu hiyo imejidhihirisha kwenye mbio za Serengeti Fiesta 2013,
ambapo muda mwingi wamekuwa wakishirikiana kwenye kazi zao za muziki na
hata kupeana lifti na kupanda gari moja jambo ambalo hapo mwanzo
lilikuwa haliwezekani.
Rais wa Manzese, Hamad Ally ,upande wa kulia ‘Madee’. akiwa na Raisi wa wasafi Diamond platnumz upande wa kushoto
Agosti 23, mwaka huu wasanii hao walitinga jijini Tanga pamoja
wakitokea Dar ambapo Nay wa Mitego ndiye aliyekuwa amepewa lifti kwenye
gari ya Madee, bila hiyana Nay alisisitiza kwamba wamemalizana
kimyakimya.“Yale yalikuwa mambo ya jukwaani zaidi, tumeyamaliza, kwa sasa tuko poa,” alisema Nay.
0 comments:
Post a Comment