Wiki chache zilizopita Joh makini, G-Nako, Vanessa, Jux, Nahreel na
Aika walienda Afrika Kusini kwa pamoja, na haikufahamika kwa haraka
kilichowapeleka licha ya watu kuhisi wameenda kushoot video.
Kwasababu wakati huo ndio wimbo mpya wa Nikki Wa Pili ‘Safari’ ambao
amewashirikisha hao wote waliokwenda South ulikuwa umetoka, wengine
walidhani huenda wameenda kushoot video ya wimbo huo lakini tatizo
likawa moja, kwenye safari hiyo alikosekana Nikki hivyo ikabaki kuwa
kitendawili.
Nikki Wa Pili amezungumza na Bongo5 na kuelezea madhumuni ya safari hiyo.
“Jux kuna wimbo wake alifanya na Joh Makini alikuwa anaenda kushoot
South Africa, Vanessa pia alikuwa anaenda kwaajili ya shughuli zake za
kikazi, kwahiyo tukaona sisi kama weusi pia tutumie nafasi hiyo
kwasababu kina Vanessa tayari kule wana pakuanzia.” Alisema Nikki Wa
Pili
Joh Makini na rapper K.O wa Afrika Kusini
“Kila siku tumekuwa tukitaka kujaribu kufungua milango mingine mipya
tofauti […] tukaona ni vizuri tujiunganishe Joh Makini na G-Nako waende
waangalie connection za media kubwa, MTV, Channel O, Trace. Joh Makini
pia alikuwa anataka kufanya collabo na wasanii wa kule K.O, AKA, Khuli
Chana kwahiyo aende akatafute mawasiliano na hawa watu na aangalie
uwezekano ni upi.”
Matunda ya connection hizo, XO imeanza kuchezwa na kituo cha Nigeria SoundCity
“Na pia alifanikiwa kupeleka video yake MTV ya XO, SoundCity na
yenyewe, Channel O pia, kwahiyo naweza nikasema kuwa Joh Makini kwenda
zake kule amefanikiwa kutengeneza link na artist wa kule na industry ya
kule amefanya video pia na Jux, na pia ameweza kujua nini kinahitajika
na nini kinawezekana kwahiyo saizi chochote akitaka kufanya labda ni
video ni collabo au kutuma nyimbo ana sehemu ya kuanzia, ni tofauti sana
na mara ya kwanza tulikuwa hatuna uelewa, kwahiyo itatusaidia sisi
kufanya plan zetu zingine.” Alimaliza Nikki.
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment