Mume wa zamani wa msichana aliyezaa na Chris Brown amechimba mkwara
kuwa kama muimbaji huyo akiendelea na hasira zake mbele ya familia yake
ataingia kwenye matatizo makubwa na yeye binafsi.
Mtandao wa TMZ umeongea na Terry Amey – anayesema kuwa alimuoa Nia
kuanzia mwaka 2003 – 2014 na wana mtoto pamoja wa kike mwenye miaka 13
aliyedai kuwa ndio maana anataka Chris ajue kuwa hatanii.
Terry anasema alitengena na Nia baada ya kupata mimba lakini kwakuwa
alijua kuwa haikuwa mimba yake aliamua kumpa talaka. Anadai hakuwa
anajua kuwa mtoto huyo ni wa Chris.
Amey ameuambia mtandao huo kuwa anajua jinsi Chris alivyo mtu wa
hasira na anasema ni bora ajizuie akiwa karibu na Nia na watoto wake ama
kutakuwepo na madhara makubwa.
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment