Kuna barua iliyosambaa mtandaoni weekend hii inayoonekana imetoka
kwenye mamlaka ya mapato nchini, TRA ikiutaka uongozi/kampuni
inayosimamia kazi zake kuwasilisha nakala za mkataba wa makubaliano kati
yao kuhusiana na masuala ya promotion katika kipindi cha kuanzika mwaka
2010 – 2014.
Barua hiyo pia inaongeza kuwa: Unatakiwa pia kuwasiliasha vielelezo
vya ushahidi kuhusiana na huduma iliyofanyika na kiasi cha fedha
kilicholipwa kulingana na ajira ya Abdulmalik Naseeb.”
Hata hivyo uongozi wa Diamond umedai kuwa barua hiyo nao wameiona kupitia mtandaoni lakini haijawafikia mkononi.
“Tunasikia tu kwenye mitandao hatuna taarifa nayo, maana
hawajawasiliana na sisi,” amesema Salam, mmoja wa mameneja wa Diamond
Platnumz.
“Inashangaza kuona kitu kwenye mitandao bila ya kuambiwa mhusika
mkuu, tumechukulia kama changamoto zilizopo kwenye maisha,” ameongeza.
Diamond bado yupo nchini Nigeria alikoenda kutumbuiza kwenye ‘The Africa Magic Viewers’ Choice Awards 2015’.
Home / News
/ Uongozi wa Diamond waongelea tetesi za Barua ya TRA Inayo husu uongozi huo pamoja na Diamond mwenyewe
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment