Nikki wa Pili Ageukia Siasa, Ajipanga Kisawa Sawa

 
Mwanamuziki wa kundi la Weusi, Nikki wa Pili amefunguka kuja na kampeni ya ‘Uchaguzi kwa Amani’ ili kuweza kuwahamasisha vijana kushiriki uchaguzi mkuu kwa amani.
Nikki wa Pili amesema kuwa wazo hilo limemjia baada ya kuona tangu mwaka 1995 vurugu zimechukuliwa kama sehemu ya kampeni hivyo kampeni hiyo itasaidia kuwahamasihsa watanzaniakushiriki uchaguzi wa 2015 kwa amani.
Amesema kuwa tangu mwaka 1995 watu wamekuwa wakihamasishwa kushiriki katika uchaguzi kupata haki ya kupiga kura lakini hakuna kampeni zilizofanywa za kuwaelimisha changamoto za vurugu na kuongeza kuwa kwa kuwaelimisha kutawasaidia sana kufanya uchaguzi wa amani.
Msanii huyo kutoka mkoani Arusha ameongeza kuwa walengwa wakubwa wa kampeni hiyo watakuwa ni vijana kwahiyo wataanza kuongea na vijana wenzao kuwa demokrasia ni malumbano ya hoja, siyo malumbano ya vikundi, kwa hiyo wasimtazame mtu na chama chake, bendera yake, na kuongeza kuwa mtu atazamwe kwa hoja na ajibiwe kwa hoja.
Nikki wa Pili amesema wameshaanza kuhamasisha kupitia mitandao ya kijamii na wameshaanza kutoa makala kwenye maazeti, mahojiano kwenye redio na endapo wahisani wakitokea watatembea nchi nzima.
Share on Google Plus

About ahmed

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment