KAULI MPYA YA ZITTO YAWATIA HOFU WABUNGE WENGI WAHOFIA KUPOTEZA MAJIMBO YAO

  KAULI MPYA KUTOKA KWA ZITTO KABWE“Wakati wa sakata la Escrow bungeni, kuna mjumbe mmoja wa PAC aliitwa na vinara wa watuhumiwa wa Escrow na kutakiwa kusema uongo bungeni kuhusu mimi kwa ahadi ya kupewa donge nono, mjumbe huyo alikataa, na hapo ndipo vinara hao wa Escrow wakaapa kutenga Shilingi Milion 500 kwa kila jimbo la kila mjumbe wa PAC kuhakikisha kuwa wajumbe hao wote hawarudi bungeni.
Kwahiyo nahisi kuwa hiki kilichonitokea sasa ni sehemu ya mkakati huo maana sakata la escrow limegusa wengi, hadi majaji wamo.”
“Kama Katiba ingebadilishwa kabla ya uchaguzi mkuu 2015 na ikaruhusu mgombea urais mwenye umri chini ya miaka 40, ningegombea urais, nahitaji kuongoza nchi, kwa ubunge imetosha, lakini kwa kuwa haiwezekani, nitagombea ubunge lakini si Kigoma Kaskazini, nitatafuta jimbo linguine la kugombea ili nao nikawatumikie, Kigoma Kaskazini nimeshafanya kila kitu, sitakuwa na jipya”
Hajasema atagombea kupitia chama gani, je, wewe ungependa agombee kwa chama gani, jimbo gani na nini maoni yako kuhusu kauli hii?
Share on Google Plus

About ahmed

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment