Viongozi wa ligi ya La Liga Real
Madrid siku ya jumamosi waliona cha mtema kuni waliposakamwa mabao 4
bila jibu na wapinzani wao Atletico Madrid katika mechi ya Derby
iliochezwa katika uwanja wa Vincente Calderon.
Hatahivyo mabeki hao hawakuweza kuhimili kishindo cha mashambulizi ya mabingwa wa ligi Atletico Madrid.
Mabao ya haraka yaliofungwa na Tiago,Saul Niguez yaliiweka Atletico kifua mbele katika kipindi cha kwanza,kabla ya mabao mengine mawili yaliofungwa katika kipindi cha pili na Antoine Griezman na Mario Mandzukic kupiga msumari wa matumaini ya Real.
Baadaye wachezaji pamoja na mashabiki wa Atletico walisherehekea sana ushindi huo.
0 comments:
Post a Comment