NUSU FAINALI AFCON KATI YA GHANA NA EQUATORIAL GUINEA YAGEUKA UWANJA WA VITA

Helkopta ya polisi ikijaribu kutuliza ghasia wakati wa mechi kati ya Ghana na wenyeji Equatorial Guinea jana.
Wachezaji wa Ghana wakitolewa uwanjani chini ya ulinzi mkali baada ya vurugu kutokea.
Polisi wakituliza ghasia za mashabiki kwenye Uwanja wa Malabo.
Polisi wakipambana na mashabiki.
Helkopta ikidumisha ulinzi uwanjani.
Chupa za maji zikirushwa uwanjani wakati wa vurugu.

MECHI ya pili ya nusu fainali ya michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) kati ya Ghana na wenyeji Equatorial Guinea kwenye uwanja wa Malabo jana usiku ilivurugika baada ya mchezo huo kusitishwa kwa zaidi ya dakika 30 kutokana na ghasia za mashabiki.

Mashabiki waliokuwa jukwaani waliwarushia chupa za maji wachezaji waliokuwa uwanjani huku polisi wa kuzuia ghasia sambamba na helikopta iliyokuwa ikiruka juu ya uwanja wakijaribu kuwatuliza mashabiki hao.

Vurugu uwanjani hapo zilikithiri katika kipindi cha pili cha mchezo kati ya Ghana na Equatorial Guinea.

Mpaka vurugu zinatokea uwanjani hapo, Ghana tayari ilikuwa kifua mbele kwa mabao 3-0 ambapo kwa matokeo hayo, Ghana imetinga fainali na itacheza dhidi ya Ivory Coast siku ya Jumapili.
Ushindi huo wa Ghana haukuwafurahisha mashabiki wa wenyeji, ambao walikuwa na matumaini makubwa kuona timu yao ikicheza fainali dhidi ya Ivory Coast.

Ghana ilianza kujipatia mabao yake kupitia kwa Jordan Ayew akifunga katika dakika ya 42 kwa njia ya penalti, Wakaso Mubarak dakika ya 45 na Andre Ayew akitupia la tatu katika dakika ya 75 ya mchezo.

Bao hilo la tatu ndilo lililozidisha fujo uwanjani hapo kwa mashabiki wa Equatorial Guinea kuwarushia chupa za maji wachezaji kiasi cha mpira huo kusimamishwa kwa muda mrefu
Share on Google Plus

About ahmed

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment