MWANAFA, LINAH WADENDEKA KWEUPEEE
Katika hali ya kushangaza hivi karibuni wanamuziki Hamisi Mwinjuma ‘MwanaFA’ na Estelina Sanga ‘Linah’, waliamua kudendeka hadharani mchana kweupee na kuwaacha watu wamepigwa butwaa.
Tukio hilo lilitokea juzikati ndani ya Uwanja wa Namfua mjini Singida wawili hao walipokuwa kwenye shoo ya Fiesta ambapo katika kusaka mzuka wa mashabiki, Linah alimsogezea uso FA na bila hiyana mahaba yakachukua nafasi.
Kufuatia tukio hilo, baada ya shoo mwandishi wetu alimfuata FA ili kumuuliza kulikoni aliamua kufanya vile ambapo hakutoa ushirikiano ila Linah alisema, hakuona shida kwani si jambo la ajabu sana kwake hasa linapokuja suala la burudani.
0 comments:
Post a Comment