Nigeria kuishitaki Schalke kwa FIFA

Shirikisho la soka Nigeria limesesema litaishitaki klabu ya Schalke ya Ujerumani kwa Fifa baada ya klabu hiyo kukataa kumruhusu mshambulizi Chinedu Obasi kushirki michuano ya kufuzu kombe la mataifa ya Afrika mwaka 2015.
Hata hivyo klabu ya Schalke imesema kuwa sababu ya kukosa kumruhusu mchezaji huyo kuondoka ni kwamba pasi yake ya usafiri iko katika ubalozi huku viza yake ikitayarishwa kabla ya kuanza kwa michunao ya klabu bingwa Ulaya.
Afisa wa habari wa Super Eagles Ben Alaiya ameambia BBC kwamba wana mechi mbili ambazo tayari zimeidhinishwa na Fifa.
"nchi yetu ina haki ya kukabidhiwa mchezaji wake Chinedu Obasi kwa michuano ya kufuzu kwa kombe hilo. ''
Nigeria ambao ni mabingwa wa Afrika, watamenyana na Congo mnamo tarehe sita Septemba. Siku nne baadaye watatoana kijasho na Afrika Kusini. Nigeria imekasirishwa na
Schalke kuhusu mchezaji wake Obasi.
Vilabu hushurutishwa kuwaruhusu wachezaji wa kigeni kuchezea nchi zao katika michunao ya kimataifa pindi wanapotakiwa na nchi zao kucheza.
Klabu hiyo ya Bundesliga inamtaka Obasi, kucheza dhidi ya Borussia Monchengladbach katika ligi hiyo na mechi itakayochezwa dhidi ya Chelsea katika michunao ya klabu bingwa Ulaya tarehe 13 na 17.
Alaiya aliongeza kusema kuwa mchezaji anapaswa kurejea kushirki majukumu ya kimataifa pindi anapohitajika.
"katibu wa timu amefanya awezalo na sasa tutachukua hatua kwa kushitaki Schalke kwa Fifa. ''
Wakati huohuo Nahodha wa Nigeria amejiondoa katika mechi mbili za kufuzu kwa michuano ya taifa bingwa Afrika.
Share on Google Plus

About ahmed

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment