Mjusi Kafiri watano waliopelekwa katika anga ya juu kama sehemu ya utafiti kuhusu maisha yao na wanavyojamiiana wamefariki.
Shirika la uchunguzi wa nga za juu la Urusi,
limesema kuwa Mjusi Kafiri hao huenda walifariki kutokana na baridi kali
baada ya mtambo wa Satelite waliokuwa ndani kuharibika.''Tunaweza kusema kwa uhakika kuwa Mjusi kafiri hao walifariki wiki moja kabla ya Satelite kutua kwa sababu miili yao ilikuwa imekauka sana,'' alisema afisa kutoka katika kituo cha utafiti wa matibabu matatizo ya kibayolojia.
Shirika la utafiti wa nga za juu la Urusi, bado halijaeleza sababu ya wanyama hao kufariki ingawa inaaminika kuwa huenda ilitokana na kuharibika kwa mtambo wa Satelite.
Hata hivyo baadhi ya Nzi waliosafiri kwenye mtambo huo kama sehemu ya utafiti uliokuwa unafanywa waliponea na hata kuzaana.
Mtambo huo ulianza safari kwenda juu tarehe 19 Julai na ulitarajiwa kukamilisha utafiti kwa kipindi cha miezi miwili, ingawa ulifanya kazi kwa siku 44 pekee kabla ya kurejea ardhini.
0 comments:
Post a Comment