KITUO CHA SHERIA, HAKI ZA BINADAMU CHATOA TAARIFA YA KAMPENI YA PILI YA GOGOTA

Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC, Dk. Helen Kijo-Bisimba akizungumza jambo mbele ya wanahabari (hawapo pichani).
Wadau…
Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC, Dk. Helen Kijo-Bisimba akizungumza jambo mbele ya wanahabari (hawapo pichani).
Wadau na waandishi wa habari wakisikiliza taarifa ya LHRC.
Mwanasheria wa kituo hicho, Harold Sungusia (kulia), Dk. Helen Kijo-Bisimba (katikati)  na Mratibu Dawati la Katiba, Anna Henga, wakisikiliza maswali ya wanahabari (hawapo pichani).
KITUO cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kimetoa taarifa ya  kampeni ya pili ya Gogota ya kusambaza uelewa wa rasimu ya pili ya katiba kwa wananchi ambayo ilizinduliwa 19 Agosti 2014 kwenye  ukumbi wa  Mlimani City ambapo mgeni rasmi alikuwa Joseph Butiku.
Akielezea taarifa hiyo mbele ya waandishi wa habari leo ofisini kwake, Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC, Dk. Helen Kijo-Bisimba, alisema baada ya uzinduzi huo wafanyakazi wa kituo hicho walitawanyika mikoani kwa ajili ya kutoa elimu ya rasimu ya pili ya katiba.

Share on Google Plus

About ahmed

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment