Kuna taarifa zimeendelea kusambazwa kwenye mitandao ya kijamii zikiwa
na maelezo kuwa: " Serikali kupitia Shirika la Elimu Tanzania, TPDC kwa
ushirikiano na kampuni za oil and gas, wanatarajia kuajiri vijana
wapatao 500 katika sekta hii mpya Tanzania kuanzia mwezi Januari na
Machi 2015, hivyo wameandaa crush program itakayoanza 6 Oktoba 2014.
Walengwa ni vijana wenye elimu ya form 4 na form 6 ambao watasoma
kwa miezi 6 na kupelekwa kwenye ajira moja kwa moja baada ya
kuhitimu!..kwa wale wenye elimu kuanzia diploma watasoma kwa miezi 3,
kozi ya oil and gas management!...Ada
kwa kundi la kwanza ni tshs 1,150,000 na kundi la pili ni Tsh 550,000.
Kwa yeyote mwenye kuhitaji fursa hii akachukue fomu Shirika la Elimu
Tanzania, application form ni Tsh 20,000 na deadline ni tarehe 30
Septemba…
Kuna
taarifa zimeendelea kusambazwa kwenye mitandao ya kijamii zikiwa na
maelezo kuwa: " Serikali kupitia Shirika la Elimu Tanzania, TPDC kwa
ushirikiano na kampuni za oil and gas, wanatarajia kuajiri vijana
wapatao 500 katika sekta hii mpya Tanzania kuanzia mwezi Januari na
Machi 2015, hivyo wameandaa crush program itakayoanza 6 Oktoba 2014.
Walengwa ni vijana wenye elimu ya form 4 na form 6 ambao watasoma
kwa miezi 6 na kupelekwa kwenye ajira moja kwa moja baada ya
kuhitimu!..kwa wale wenye elimu kuanzia diploma watasoma kwa miezi 3,
kozi ya oil and gas management!...Ada kwa kundi la kwanza ni tshs
1,150,000 na kundi la pili ni Tsh 550,000. Kwa yeyote mwenye kuhitaji
fursa hii akachukue fomu Shirika la Elimu Tanzania, application form ni
Tsh 20,000 na deadline ni tarehe 30 Septemba 2014".
TPDC inapenda kuwaeleza Watanzania kuwa habari hizo si za kweli na
kwamba TPDC haijafanya makubaliano yoyote na Shirika la Elimu kuhusu
suala hilo. TPDC inawaasa Watanzania kuchukua tahadhari ya matangazo ya
aina hiyo na inapotokea, tafadhali wasiliana nasi kwa namba za simu
zilizooneshwa hapo nchini.
IMETOLEWA NA
ITENGO CHA MAWASILIANO,
SHIRIKA LA MAENDELEO YA PETROLI TANZANIA
BWM Pensions Towers, Tower A,
Junction of Azikiwe /Jamhuri Streets
P. O. Box 2774,
Tel: +255 22 2200103/4
Dar-es-Salaam, Tanzania
0 comments:
Post a Comment