USAJILI wa mafowadi uliofanywa na mahasimu wa Simba kwenye Ligi Kuu Bara, Yanga, umeitisha klabu hiyo na maofisa wake wameamua kupiga kambi jijini Kigali kwenye Kombe la Kagame mpaka impate beki wa maana.
Simba ambayo Mwenyekiti wake wa Kamati ya Usajili,
Zacharia Hans Poppe yupo mjini Kigali, tayari imempata na kumtanguliza
Unguja, Zanzibar beki wa Telecom ya Djibout ambaye ni raia wa Burundi,
Butoyi Hussein na jana Jumatano jioni alianza matizi na timu.
Kiongozi huyo alisema kwamba wanahitaji kufanya
usajili wa beki imara wa kupambana na fowadi kama ya Yanga yenye
straika, Mbrazil Genilson Santos ‘Jaja’, Emmanuel Okwi pamoja na Azam
iliyosajili washambuliaji kutoka Ivory Coast, Haiti na Burundi.
Hans Poppe ameiambia Mwanaspoti jijini Kigali
kwamba wameangalia ufanisi wa kikosi kwenye mechi ya Simba Day dhidi ya
Zesco wakagundua kwamba wanahitaji kufanya mabadiliko haraka.
Mbali na hilo pia kigogo huyo mwenye ushawishi
mkubwa Msimbazi, alisema wanataka kutafuta beki imara ili wampe mkono wa
kwaheri, Donald Mosoti ambaye amewaambia wamuache aende Qatar.
“Mosoti anataka kwenda Qatar ndio maana tunatafuta
beki wa maana kwenye haya mashindano, tukifanikiwa tu tunamuacha Mosoti
aende zake. Yule Butoyi tumemtanguliza kwamba kocha amuangalie
mazoezini, akikubaliana naye sawa tutamsainisha rasmi,” alisema.
“Lakini vinginevyo inabidi tuendelee kutafuta
mwingine tena. Tunataka kuwa na beki katili na mbishi asiyekubali
matokeo kirahisi, ukiangalia wapinzani wetu wameisuka upya safi yao ya
ushambuliaji hatutaki kuwaangalia wao sana, lakini tunataka kuwa tayari
na aina yoyote ya washambuliaji wasumbufu.”
Mosoti aliiambia Mwanaspoti jana kwamba yupo tayari kuondoka dakika yoyote kama uongozi ukimruhusu.
ZA MOSOTI
Kocha Patrick Phiri, ameuagiza uongozi wa Simba
kumpelekea video za mechi ya Nani Mtani Jembe na nyingine mbili
walizocheza na Yanga msimu uliopita ili kuangalia kiwango cha wachezaji
wake wawili, beki Mkenya Donald Mosoti na kiungo Jonas Mkude ambaye kwa
sasa ni majeruhi.
Awali, Mosoti aliomba kuvunja mkataba wa timu hiyo
ili aende kucheza katika moja ya timu alizopata Qatar, hivyo huenda
ujio wa Hussein ukamfanya Mosoti kuondoka ambapo yeye amekiri kuwa
atakuwa tayari kuondoka muda wowote.
0 comments:
Post a Comment