January 1 2016 timu ya Simba yaanza vyema mchezo wake wa kwanza wa Kombe la Mapinduzi 2017 dhidi ya timu ya Taifa Jang’ombe katika uwanja wa Amaan huko visiwani Zanzibar, katika mchezo huo Simba walifanikiwa kupata ushindi wa goli 2-1.
Dakika ya 28 Simba walipata bao la kwanza kupitia kwa kiungo wao, Mzamiru ambaye alimalizia kazi nzuri iliyofanywa na Mwanjale ambaye alipiga shuti kali kutoka nje ya 18 likagonga mwamba na kurejea uwanjani kisha Mzamiru akamalizia kazi.
Na mnamo dakika ya 28 Juma Luizio anaipatia Simba bao la pili, anawatoka walinzi wa Jang'ombe na kupiga shuti kali linalojaa wavuni moja kwa moja.
Dakika ya 76 Beki wa kati wa Simba, Lufunga aliiandikia Taifa Jang'ombe bao la kwanza na la pekee kwakujifunga wakati akiwa katika harakati za kuokoa mpira wa kona, aliruka juu ili kuupiga kichwa lakini badala ya kuokoa akausukumiza langoni kwake na kuwafaidisha maadui.
Hichi ndio kikosi cha simba dhidi ya Jang'ombe
1. Daniel Agyei2. Hamad juma
3. Mohammed Hussein
4. Novaty Lufunga
5. Method Mwanjale
6. James Kotei
7. Shiza Kichuya
8. Muzamiru Yasin
9. Juma Luizio
10. Saidi Ndemla
11. Jamali Mnyate
Huku michezo mingine ikienda kama hivi........
- African Lyon 0 - 0 JKT Ruvu Stars
- Toto Africa 2 - 1 Stand United
0 comments:
Post a Comment