Je kweli uko tayari kuingia kwenye mahusiano? Kama utajikuta
unaangukia kwenye mojawapo ya vitu vitakavyotajwa hapo chini,
inamaanisha kuna kazi ya ziada inatakiwa ifanyike kwako ili uwe na
mahusino yenye afya au mahusiano yenye malengo na yatakayodumu muda
mrefu.
Kama unajiona huvutii
Hii inawahusu hasa wanawake au dada zetu. Wao hupenda kuangalia
mwonekano wa nje na kufikiri kwamba ukiingia kwenye mahusiano unafikiri
mtu mwingine atakwambia wewe ni mzuri au una mvuto, hapo unakuwa
umekosea. Ukweli ni kwamba hakuna mtu atakayekuambia wewe ni mzuri kama
wewe mwenyewe hujitambui na kama hujiamini. Wewe ni mtu wa thamani na
hakuna atakayeweza kufanana na wewe kwasababu uko peke yako. Unapoingia
kwenye mahusiano uwe mtu ambaye unatambua wewe ni nani na thamani yako
iko wapi. Ukitegemea watu wengine wakuthaminishe, watakuweka kwenye
mazingira mabaya au kukuharibu kwa kukulazimisha ufanye wanavyotaka wao
au uonekane wanavyotaka wao hivyo unajikuta unapoteza utu wako na hata
kuharibu mwili wako.
Kama wewe ni mtu wa visasi na husamehi watu wengine
Huwa unasema umemsamehe mtu lakini hiyo ni ya mdomoni tu, moyoni bado
unapanga namna yakuja kulipiza kisasi. Umekuwa unafikiria vitu
vilivyotokea miaka ya nyuma na ndio sababu hata sasa kuna watu bado una
vinyongo nao. Hii pia inaweka kasoro kwenye mahusiano yako na mpenzi
wako wa sasa. Utajikuta mambo mengi unavyochukulia unakumbuka watu wa
nyuma walichokufanyia. Inachokubidi kufanya ni kuruhusu kinyongo
kiondoke na uponye moyo wako kwa kwenda hatua nyingine bora zaidi.
Wewe ni mtu usiyetaka kubadilika
Kila wakati unasema utafanya vizuri lakini haufanyi chochote, iwe kwenye
taaluma yako au biashara na hata imani. Unajua kabisa una mapungufu
fulani ambayo unatakiwa kuyafanyia kazi lakini hauyafanyii kazi na mambo
yanapotokea unatafuta mtu wa kumlaumu. Kila siku lazima uchukue muda wa
kushughulikia tabia zako, hulka na kujitambua vizuri ili uwe mtu wa
kuambukiza matendo kwa watu wengine, kuna tatizo kwako mwenyewe.
Huwa huchagui wanaume wa kwenda nao
Kwa kifupi unaweza ukaitwa jalala au hauna mwelekeo ni kama hujui nini
unataka. Umekuwa ni mtu ambaye marafiki zako wanakuuliza kwanini uko na
mtu huyu au huoni kwamba huyu mtu ana matatizo au ana hiki na hiki na
wewe huna majibu? Hapa sizungumzii wale wenye wivu bali nazungumzia kwa
wale ambao wanajua umeingia mikono ambayo sio salama na wala hakuna
malengo ya maisha ya baadaye hapo. Kumbuka watu wengi wanaweza kuonekana
wanakuzungumzia sana kuhusu mtu uliyenae ni kwa sababu ya viwango vyako
ulivyosema vinatofautiana na unachokifanya au maamuzi unayochukua sasa.
Ni wakati wa kujichunguza mwenyewe na kujua unatakiwa kuwa wapi na nani
na kwasababu gani, usifanye mambo bora liende au kufuata mkumbo. Maisha
ni mafupi sana hivyo, hivyo fanya maamuzi sahihi ambayo yatakusaidia
kuishi kila siku ukiwa na furaha na amani.
Hauna furaha
Kama hauna furaha sasa hivi, kwanini unaruhusu kuingia kwenye mahusiano
mtu ambaye aje kushughulikia matatizo yako ya kutokuwa na furaha? Hakuna
mtu ambaye anataka kuingia kwenye mahusiano na mtu ambaye ni mzigo
kimawazo au kihisia, lazima mahusiano hayo yatakuwa na matatizo kwani
wewe furaha yako itategemea sana yule mwenzako hivyo unakuwa unamnyonya
kihisia. Ingia kwenye mahusiano ukiwa na furaha au hisia zako ziko
sawasawa inamaanisha kwamba uko vizuri kiasi kwamba usiwe mzigo upende
wa pili, kila dakika umenuna, una mawazo n.k. Fanya upendo wako
hakikisha unatafuta furaha kabla ya kuingia kwenye mahusiano, hivyo
badilisha mtizamo wako na ufanye mambo yenye akili. Kumbuka tuko kwenye
jamii ambayo wakati wote huwa hatupendi kuonekana tuna tatizo fulani,
ila kuna matatizo makubwa ndio maana mambo mengi hayaendi kama
yalivyokusudiwa.
Ninajua unajua mambo mengi hivyo nimetoa kidogo kuweza kusaidia pale
ambapo pamepungua. Jambo la msingi ni kuwa ufahamu wako ukikua na
kubadilika unaweza kubadilisha hali ya mambo yanavyokwenda na kuwa bora
zaidi. Majibu yote ninaamini uko nayo ni suala tu la kuyafanyia kazi.
Home / Bongo yetu /
Entertainments /
isikupite /
Utaipenda
/ Viashiria vitano vinavyokuonyesha kwamba hutakiwi kuingia kwenye mahusiano ya kimapenzi
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment