Filamu ya Fast & Furious 7 imezinduliwa April 3 duniani kote.
Tanzania ni moja ya nchi zilizoionesha filamu hiyo kwa mara ya kwanza.
Hamu kubwa ya mashabiki wa filamu nchini, imeyafanya majumba ya
sinema jijini Dar es Salaam kuuza tiketi nyingi kuliko kawaida. Meneja
wa Century Cinemax iliyopo Mlimani City jijini Dar es Salaam, Haji
Madoweka, ameiambia Bongo5 Ijumaa hii kuwa tiketi za kuangalia filamu
hiyo zimeisha kwa siku za Ijumaa, Jumamosi na Jumapili.
Madoweka amedai kuwa filamu hiyo ilikuwa ikisubiriwa kwa hamu na
mashabiki wake na ndio maana tiketi zimeisha mapema kiasi cha kumfanya
aongeze chumba kingine kwaajili ya kuwaruhusu watu wengine kuitazama.
Amesema kwa siku huonesha filamu mpya mara tano katika muda unaoanzia
saa mbili asubuhi hadi saa saa nne usiku, lakini kutokana na watu wengi
kununua tiketi, imewalazimu kuongeza show nyingine ya saa tano usiku.
“Kwa kawaida huwa hatuwezi kujaza siti zote lakini filamu hii
imetufanya tuongeze show moja tena ya kuanzisha saa tano usiku,” amesema
Madoweka. “Hapa ili kupata nafasi nzuri labda kuanzia Jumatatu.
Amedai kuwa kifo cha Paul Walker, kilichotokea November mwaka 2013 ni
sababu moja wapo iliyoifanya Furious 7 ivutie watu wengi wanaotaka
kujua alichomalizia kuigiza kabla mauti hayajamkuta.
Sam ni mmoja wa mashabiki wa filamu hiyo ambaye ameiambia Bongo5 kuwa
alinunua tiketi mapema zaidi ili kuitazama Ijumaa hii. “Naipenda Fast
and Furious sababu ya yale mashindano ya magari, napenda sana driving,”
amesema Sam.
“Kingine nataka kufahamu Paul Walker alivyoigiza.”
Kwa upande wake Janet Loveness aliyeshindwa kuitazama filamu hiyo leo
baada ya kukosa tiketi amedai ni Vin Diesel ndiye anayemvutia kwenye
filamu hiyo. “Napenda uigizaji wa Vin Diesel, nataka kujua alichofanya
kwenye Furious 7,” Janet ameiambia Bongo5.
Pamoja na kufariki kwa muigizaji wake muhimu Paul Walker mwaka juzi,
filamu ya Fast & Furious 7 inatarajiwa kuingiza makadirio ya faida
ifikayo dola bilioni 1.37.
Furious 7 inaweza kuingiza dola milioni 119 za mauzo ya tiketi katika
weekend yake ya kwanza na dola milioni 283 kwenye majumba ya sinema
nchini Marekani na Canada kwa mujibu wa BoxOffice.com.
Hiyo itafanya Fast & Furious kuwa filamu ya mfululizo hiyo yenye
mafanikio zaidi kuliko zote. Kwa pamoja filamu za kwanza sita ziliingiza
dola bilioni 2.38.
Walker alifariki akiwa na umri wa miaka 40 kwa ajali mbaya ya gari November 2013.
Home / Entertainments /
isikupite /
movies /
Utaipenda
/ Uzinduzi wa Filamu ya Fast & Furious 7 wafunuka Duniani kote Wavunja Record
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment