Charles Hillary wa BBC kurejea Tanzania na kujiunga na Azam TV


Ngome ya kituo cha Azam TV inaendelea kuimarishwa, baada ya kuzinduliwa kwa studio kubwa na za kisasa za kituo hicho zilizogharimu zaidi shilingi bilioni 56, inadaiwa kuwa kampuni ya Azam Media itamrejesha nyumbani mtangazaji mkongwe wa BBC, Charles Hillary kwaajili ya kuja kujiunga na Azam TV. hillary2
Mchambuzi maarufu wa soka Edo Kumwembe ambaye pia hufanya uchambuzi kwenye kituo hicho, amepost taarfia hiyo kwenye akaunti yake ya Facebook kwa kuandika:
“….Mtangazaji maarufu wa BBC, Charles Hillary, anarudi nyumbani kujiunga na kituo cha Azam TV…..welcome home LEGEND….”
Hillary
Hata hivyo chanzo kingine cha kuaminika cha ndani ya Azam TV kimethibitisha kuwa Hillary anarudi kujiunga na kituo hicho.
Share on Google Plus

About ahmed

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment