Mimi ni bonge moja la comedian – Ommy Dimpoz

Muziki ukifeli, Ommy Dimpoz ana kipaji kingine kitakachomwezesha kupata mkate wake wa kila siku – uchekeshaji!
Dimpozi
Akiongea na kipindi cha The Chart cha Times FM, Ommy Dimpoz alisema ana uwezo mkubwa wa kuchekesha pia.
“Unajua mimi ni comedian sana yaani,” alisema. “Unaweza kukuta nina marafiki wengine wengi tofauti na wanamuziki kwa sababu tu ya vituko vyangu. Sometimes jamaa anakupigia simu ‘ibuka maskani’ ili umchekeshe tu sababu anajua ukifika pale atacheka sana.”
Katika hatua nyingine Ommy aliwataka mashabiki wake kutomjaji kwa vile wanavyomuona kwenye mitandao bali waangalie maisha yake halisi.
Share on Google Plus

About ahmed

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment