YALIYO JIRI KATIKA MECHI YA SIMBA NA YANGA

Simba imeendeleza ubabe wake dhidi ya watani zao wa jadi Yanga baada ya jioni ya leo kuifunga bao 1-0 kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam katika mchezo wa ligi kuu Tanzania Bara.
simba2
Goli pekee la Simba lilifungwa na mshambuliaji wa kimataifa kutoka Uganda Emmanuel Arnold Okwi katika kipindi cha pili.
simba
Okwi alifunga goli hilo dakika ya 52 kwa shuti la umbali wa mita 22 baada ya pasi ya Said Ndemla aliyetokea pembezoni mwa uwanja na kumtungua kipa Ali Mustapha ‘Barthez’.
simba3
simba4

Kikosi cha Simba:- Ivo Mapunda,Hassan Kessy,Mohamed Hussein ‘Tshabalala’,Hassan Isiaka, Juuko Murshid, Abdi Banda/Simon Sserunkuma, Ramadhan Singano ‘Messi’,Jonas Mkude, Ibrahim Haji/Elias Maguri,Said Ndemla, Emmanuel Okwi.

Kikosi cha Yanga:- Ally Mustapha Barthez, Mbuyu Twite,Oscar Joshua, Nadir Haroub Cannavaro, Kelvin Yondan,Siad Juma, Simon Msuva,Haruna Niyonzima,Hamis Tambwe,Danny Mrwanda, Mrisho Ngassa/Kpah Sherman.
Share on Google Plus

About ahmed

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment