Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limetangaza viingilio vya mchezo wa siku ya jumapili kati ya Simba SC na Young African utakaofanyika kwenye dimba la Uwanja wa Taifa kuanzia majira ya saa 10 kamili za jioni
Mchezo huo utachezeshwa na mwamuzi Martin Saanya kutoka Morogoro, akisaidiwa na Soud Lila (DSM) mshika kibendera wa kwanza, Florentina Zabron (Dodoma) mshika kibendera wa pili, Mwamuzi wa akiba Israel Mjuni (DSM), na kamisaa wa mchezo ni Ame Santimeya (DSM).
Viingilio vya mchezo huo,
VIP A
sh. 40,000,
VIP B sh. 30,000,
VIP C sh. 20,000,
Rangi ya Machungwa
(Orange) sh. 10,000, huku
Rangi ya Bluu na Kijani ikiwa ni sh. 7,000.
Tiketi zitaanza kuuzwa kesho (jumamosi) saa 2 kamili asubuhi katika vituo vya, Karume
(Ofisi za TFF), Mgahawa wa Steers (Posta Mpya), Oilcom (Buguruni),
BigBon (Kariakoo), Olicom (Ubungo), Dar Live (Mbagala), Uwanja wa
Uhuru, Kivukoni (Ferry) na Makumbusho (kituo cha mabasi).
Magari yenye vibali maalum ndiyo
yatakayoruhusiwa kuingia ndani ya uwanja siku ya jumapili kwa kupitia
barabara ya Mandela na Uwanja wa Uhuru, barabara ya Chang’ombe itafungwa
kuanzia saa 12 kamili asubuhi.
TFF inawaomba, wapenzi, washabiki na
wadau wa mchezo kununua tiketi katika vituo vilivyotajwa ili kuepuka
kuuziwa tiketi bandia, ili kuimarisha ulinzi na usalama wa mchezo,
mashabiki wenye mabegi, silaha, vilevi na chupa za maji hawataruhusiwa
kuingia navyo uwanjani.
Aidha, katika mchezo huo TFF itatoa
ujumbe maalum kupitia kwa wachezaji kuhamasisha juhudi za Taifa za
kuzuia mauaji dhidi ya watu wenye ulemavu wa ngozi (Albino).
0 comments:
Post a Comment