Mkali wa Formula One, Lewis Hamilton ahidi kuwateka mashabiki wa muziki.
Dereva huyo mwenye umri wa miaka 30 yupo kwenye mazungumzo na Jay Z ili muziki wake usimamiwe na Roc Nation, kwa mujibu wa The Sun. Chanzo kimeliambia The Sun kuwa Lewis yupo kwenye mazungumzo na wasanii wengine pia.
Kwa mujibu wa chanzo hicho, Lewis yupo serious na muziki na amekuwa akitumia muda wa studio na wasanii wakubwa. Dereva huyo anadaiwa kuwa ameshaanza kurekodi na watayarishaji wakubwa akiwemo Rodney Jerkins.
Awali Lewis alikuwa na Jay Z studio pamoja na Timbaland na BeyoncĂ© ambako Jigga alimchagulia nyimbo za kuanza nazo. “Natamani ningeweza kuchukua picha sababu ilikuwa ni moja ya wakati bora katika maisha yangu,” alisema Lewis.
0 comments:
Post a Comment