Mohammed Dewji ndiye mtu tajiri zaidi nchini Tanzania, kwa mujibu wa orodha ya mwaka 2015 ya mtandao wa Forbes wa mabilionea 32 barani Afrika.
Awali ni Rostam Aziz ndiye aliyekuwa akishikilia nafasi hiyo.
Kwa mujibu wa Forbes, Dewji mwenye umri wa miaka 39 ana utajiri wa
dola bilioni 1.3. Utajiri huo unamfanya mfanyabiashara huyo ambaye pia
ni mbunge wa Singida Mjini, kushika nafasi ya 1,500 katika orodha ya
watu matajiri duniani, nafasi ya 31 barani Afrika na nafasi ya kwanza
Tanzania.
Rostam Aziz, 50, mwenye utajiri wa dola bilioni 1 anakamata nafasi ya
1,741 duniani, nafasi ya 32 barani Afrika na nafasi ya pili nchini.
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment