Mwanasheria mkuu wa CHADEMA, Tundu Lissu ametangaza kuvuliwa rasmi uanachama kwa mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe.
Uamuzi huo umekuja baada ya chama hicho kushinda kesi dhidi ya
Zitto. Mahakama imeamua katika hukumu yake leo kuwa chama kinaweza
kuendelea na taratibu zake. Aidha, mahakama imeamuru Zitto alipe gharama
zote za kesi.
Lissu amesema uamuzi huo umetokana na katiba ya CHADEMA, inayosema
kuwa mwanachama anapofungua kesi dhidi ya chama, na kushindwa atakuwa
amejiondoa uanachama wake.
“Kwahiyo natangaza rasmi rasmi Zitto Kabwe sio mwanachama tena wa
Chadema na hii na kwa mujibu wa katiba ya chama,” amesema Lissu.
Hata hivyo Zitto ametumia Twitter kueleza kuwa hakuna na taarifa za kuitwa Mahakamani leo.
“Hatukuwa na wito wa mahakamani leo. Jaji kahamishiwa Tabora. Hatuna
taarifa ya Jaji Mpya. Mwanasheria wetu anafuatilia na atatoa statement,”
ameandika.
“Kwa sasa naendelea na kazi zangu kama kawaida. Leo nipo na EWURA
kwenye PAC. Kesho TANESCO na Alhamis Mabilioni ya Uswizi. Kwa kazi ya
#TegetaEscrow ilivyokuwa ingeshangaza waathirika kukaa bila kujaribu
kunivuruga. Bahati mbaya sana sivurugiki. Ni Kazi tu.”
Novemba 22 mwaka jana, Zitto alisimamishwa unaibu Katibu Mkuu wa
Chadema na unaibu kiongozi wa upinzani bungeni baada ya kutuhumiwa
kuhusika na njama za kukihujumu chama hicho.
Zitto pia aliweka pingamizi mahakamani kuzuia kikao cha kamati Kuu
kumjadili. Hoja yake ilikuwa ni kupinga kuitisha kamati kuu kabla shauri
lake kusikilizwa na baraza Kuu.
Alidai anataka mahakama iagize kamati kuu ya CHADEMA kutojadili suala lake mpaka baraza kuu likae kuamua rufaa yake.
CHANZO: EATV (Twitter), Jamii Forums
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment