Stori: Imelda Mtema/Amani
Kufuatia kauli yake ya hivi karibuni kuwa nyumba anayomiliki ilitokana
na mchango wa bwana’ke (hakumtaja jina), mama mzazi wa staa wa sinema za
Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’, Lucresia Karugila ameibuka na
kumkataa mwanaume huyo.
Kwa mujibu wa Lulu, nyumba hiyo iliyopo Kimara jijini Dar ameijenga
kwa kusaidiana na bwana’ke kwa mtindo wa pasu kwa pasu (kuchangia nusu
kwa nusu).Alisema kuwa anamshukuru Mungu kwani hadi hapo ilipofikia
ikiwa inakaribia kumalizika ameijenga kwa nguvu zake na mwanaume wake
huyo.
“Yeah! Nimejenga kwa msaada wa mwanaume wangu, tunasaidiana nusu kwa nusu,” alinukuliwa Lulu.
Pamoja na mbwembwe zote hizo za staa huyo kwa jamaa yake huyo, mama
mzazi wa Lulu ameliambia Amani kwamba hamtambui mwanaume huyo kwani
hajawahi kwenda kujitambulisha kwake pamoja na kwamba kahusika kutoa
fedha kwa ajili ya ujenzi wa nyumba hiyo.
Alifunguka: “Sijawahi kutambulishwa na Lulu kama ana mchumba.
“Kwa hiyo awe amemsaidia au hajamsaidia, mimi simtambui.
“Ingekuwa Lulu amewahi kumtambulisha kwangu kuwa huyo ndiye mchumba wake hapo sawa lakini hakuna kitu kama hicho.
“Halafu naomba utambue kwamba Lulu hawezi kumtambulisha bwana’ke au
boy friend wake kwangu, siyo heshima labda awe mchumba. Hapo kidogo
afadhali lakini mtu tu mtu, hakuna kitu kama hicho.
Kabla ya Lulu
kueleza ukweli juu ya ujenzi wa nyumba hiyo, awali kulikuwa na madai
kwamba alihongwa na mheshimiwa mmoja (jina tunalo) huku wote wakikanusha
kwa nyakati tofauti.
Hata
hivyo, kitendo cha Lulu kumiliki mjengo huo kimempa heshima kubwa
tofauti na mastaa wenzake wa kike ambao wamekuwa wakiishia kupangiwa
nyumba na kuhongwa magari yasiyo na kadi kisha kunyang’anywa na kurudia
maisha ya kawaida uswahilini.
Home / Bongo Movie /
Bongo yetu /
isikupite /
Ma Star wetu /
udaku /
Utaipenda
/ MAMA LULU AMKATAA MCHUMBA WA MWANAE
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment