KOVA APIGA MARUFUKU MAANDAMANO YA VIJANA CUF

Kamishna Kova akizungumza na wanahabari (hawapo pichani)

Wanahabari wakimsikiliza Kamishna Kova (hayupo pichani)
KAMISHNA wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar e s Salaam, Suleiman Kova leo ametoa tamko mbele ya wanahabari juu ya maandamano ya vijana wa Chama cha…
Kamishna Kova akizungumza na wanahabari (hawapo pichani)
Wanahabari wakimsikiliza Kamishna Kova (hayupo pichani)
KAMISHNA wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar e s Salaam, Suleiman Kova leo ametoa tamko mbele ya wanahabari juu ya maandamano ya vijana wa Chama cha Wananchi CUF (JUVICUF) yaliyokuwa yamepangwa kufanyika hapo kesho.
Kamanda Kova amewataka vijana wa CUF  kutoandamana  kesho na kama wataandamana jeshi hilo halitakuwa tayari kuona maandamano hayo yakifanyika .
Alisema kuwa maandamano hayo yalikuwa yamepangwa kufanyika kesho Februari 13 mwaka huu   kutoka  Buguruni, Shule ya Uhuru, Mnazi Mmoja, Mtaa wa Ohio hadi Tume ya Taifa ya Uchaguzi  na kisha Wizara ya Mambo ya Ndani ,kwa dhumuni la kuitaka Tume ya Taifa ya Uchanguzi (NEC) iongeze siku za uandikishwaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kutoka siku saba hadi siku 14, pamoja na kulaani ukiukwaji wa haki za binadamu unaofanywa na jeshi la polisi nchini.
Kova ametaja sababu za kuzuia maandamano hayo kuwa siku waliyoomba ni siku ya kazi, ambapo maandamano hayo yakifanyika yatasumbua mfumo mzima wa shughuli za jiji zima, kibiashara, huduma za afya, walemavu, watoto na n.k.
Share on Google Plus

About ahmed

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment