TAMASHA LA KISWAHILI (SWAHILI FEST) LILILOFANYIKA NCHINI MAREKANI NDANI YA WASHINGTON DC LAFUNIKA !‏

Waandaaji wa Tamasha la Kiswahili Washington DC Ndugu Patrick Kajale na Dada Finiana wakijadili jambo na ndugu Safari ambaye ndiye Mtunzi wa kile kitabu Nambari moja Amazon cha Nyayo za Obama.
Ndugu Safari Akionyesha Kitabu cha ObamaPatrick Kajale  Mwandaaji wa Tamasha la Kiswahili
Afisa usalama wa ubalozi wa Tanzania Dr Mkama akiwa na baadhi ya maofisa wa ubalozi.
Maofisa wa ubalozi wakiendelea kula nyamachoma kutoka katika banda la Safari Restaurant DC
Nyama Choma katika banda la Safari Restaurant Washington DC,Safari ni Mgahawa wa Kitanzania  uliopo katika jiji la Washington ambapo vyakula vingi vya kinyumbani vinapatikana.
Mishikaki ikiendelea kuchomwa katika banda la Safari Restaurant kwenye Tamasha la Kiswahili
Watu wakiwa mstari kwenye banda la Safari wakijipatia nyama ya motomoto kutoka kwenye grill
Mabanda mbali mbali yakitangaza shughuli zao kwenye Tamasha la kiswahili
Warembo Wakareeeeezz kutoka washington DC na Texas pia walihudhuria Tamasha hili la Kiswahili
Ice Cream au lamba lamba kama zinavyojulikana kwa kiswahili pia zilikuwepo kwa ajili ya watoto na watu wazima
Miss Malaika nae pia hakupitwa akionyesha kuwa "She is Very Confident"
Miss Temeke- CEO wa Kwetu Fashion Design akiwa katika Meza yake  baada ya kumaliza Maonyesho yake ya Mavazi ya Kitanzania.
Walimbwende  hawa katika Mavazi ya Kwetu Fashion Design.
Nguo za kina Kaka kutoka kwetu fashion Design By Miss Temeke  Patrick Kajale nae akipita katika Vazi la Kimasai
CEO Wa Kwetu Fashion Miss Temeke Akiwapungia Umati Baada yakumaliza Maonyesho yake ya Mavazi
Juu na chini ni watu mbali mbali wakiendelea kutazama mambo mbali mbali yaliyokuwa yakiendelea.
Kwa Upande wa burudani walikuwepo pia  Wasanii  Mahiri wa kizazi Kipya Wakitanzania na East Afrika kwa ujumla waishio Marekani kama AJ Ubao,Prince Herry,Max na Jumbe Mr TZ Mwanadada "Senai" Mpiga Gitaa Maarufu kutoka Afrika Mashariki anayeishi Marekani
Mikono Juu..Prince Herry akiwarusha Watazamaji kwa Ufasaha na Style yake ya lay back.Prince Herry Akifokafoka kwa hisia kali katika kile kibao chake kinachoitwa "Au Sio"
Kijana Max Ambaye watu wengi wanamwita Silent Killer aliwarusha watazamaji vilivyoJumbe Mr Tanzania aliwarusha watazamaji kwa style yake yakipekee huku Mwanamuziki AJ Ubao akimsindikiza kwa nyuma
Je waukumbuka Mchezo gani huo?....Mwakani tutaweka pia Bao.
Kwa mara ya Kwanza kabisa nchini marekani limefanyka tamasha la Kiswahili katika jiji la Washington, likijumuisha nchi zote za Afrika Mashariki na kati zinazozungumza lugha ya kiswahili.Tamasha hili liliandaliwa ili kuweza kutangaza tamaduni za Afrika Mashariki ikiwa ni pamoja na Chakula, Mavazi, Ngoma za Asili, Miziki ya Kizazi Kipya,na mambo mbali mbali ya kiasilia.
Waandaaji Wanatoa Shukrani Kwa watu wote waliojitokeza kwani hii ni mara ya kwanza kabisa Tamasha kama hili kufanyika nchini Marekani hivyo tutegemee Mambo mengi Makubwa Mwakani kwani Huu ni Mwanzo.
Share on Google Plus

About ahmed

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment