NUSU FAINALI DANSI 100% KUFANYIKA DON BOSCO JUMAMOSI‏


Meneja wa huduma na bidhaa wa Vodacom Tanzania,Liginiku Milinga(kulia)akiwaonesha waandishi wa habari(hawapo pichani)Simu aina ya Samsung E1205 yenye tochi na redio yenye thamani ya shilingi 25,000 tu.Zitakazopatikana katika Nusu fainali ya Dance 100 itakayofanyika jumamosi Don Bosco Oysterbay jijini Dar es Salaam,pamoja nae kushoto ni Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania Matina Nkurlu.
Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania Matina Nkurlu(kushoto) akiwaonesha waandishi wa habari(hawapo pichani)Simu aina ya Samsung E1205 yenye tochi na redio yenye thamani ya shilingi 25,000 tu.Zitakazopatikana katika Nusu fainali ya Dance 100 itakayofanyika jumamosi Don Bosco Oysterbay jijini Dar es Salaam,pamoja nae kulia ni Meneja wa huduma na bidhaa wa Vodacom Tanzania,Liginiku Milinga,Kikundi kitakachoshinda katika shindano hilo kitajinyakulia kitita cha shilingi Milioni 5.
Meneja wa huduma na bidhaa wa Vodacom Tanzania,Liginiku Milinga(kulia)akiwaonesha waandishi wa habari(hawapo pichani)Modem yenye ubora wa 3G inayouzwa kwa shilingi 25,000 tu katika Nusu fainali ya Dance 100 itakayofanyika jumamosi Don Bosco Oysterbay jijini Dar es Salaam,pamoja nae kushoto ni Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania Matina Nkurlu.
Na Mwandishi wetu.
Kinyang’anyiro cha mashindano yanayokuwa kwa kasi hapa nchini ya Dance 100% yanayoandaliwa  na kituo cha televisheni cha East  Africa(EATV) chini ya udhamini wa Vodacom Tanzania,yanaendelea ambapo hapo jumamosi hatua ya nusu fainali  inafanyika katika uwanja wa Don Bosco Oysterbay jijini Dar es Salaam na kushirikisha makundi 10 kutoka wilaya 3 za mkoa wa Dar es Salaam.
Makundi ya wachezaji wa miondoko mbalimbali ya muziki ambao yamefanikiwa kuingia katika kinyang’anyiro hicho mpaka sasa ni Wazawa Crew,Best Boys Crew,G.O.P,The W.T,Tatanisha Dancers,Quality Boys,Wakali sisi, Mazabe Powder,Dar Crew na The winners Crew.
Mratibu wa mashindano hayo,Happy Shamte,alisema kuwa katika kinyang’anyiro cha nusufainali hiyo watapata makundi 5 yatakayoingia  moja kwa moja kwenye fainali hapo baadaye.
“Huu ni mwaka wa tatu EATV tunaandaa mashindano haya chini ya udhamini wa Vodacom Tanzania.Kwa kweli mwaka huu mashindano haya yamekuwa na umaarufu mkubwa na ushindani wa hali ya juu na kuwavutia vijana wengi ambao hujitokeza kushiriki”Alisema Shame.
Shame, aliongeza kwamba kundi litakaloibuka na ushindi katika mashindano haya ambayo pia yamekuwa yakionyeshwa na kituo cha televisheni cha East Afrika kila jumatano saa  moja kamili usiku,litajishindia kitita cha shilingi milioni 5.
Naye Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania ambao ni wadhamini wakuu wa mashindano haya,Matina Nkurlu alisema kuwa  Vodacom itaendendelea kudhamini kwa kutambua kuwa muziki na michezo ni maeneo ambao yanaweza kutoa ajira kwa vijana na kuweza kuwakwamua kimaisha.
Alisema kuwa Vodacom inatambua kuwa jukumu la kukabiliana na tatizo la ajira hapa nchini sio la serikali peke yake bali pia ni la watu wote ikiwemo makampuni,taasisi za umma na za binafsi na ndio maana siku zote imekuwa mstari wa mbele katika kuunga mkono jitihada za kupambana na tatizo la ajira kupitia nyanja mbalimbali ikiwemo michezo , burudani na huduma mbalimbali zinazotolewa na kampuni hiyo.
“Vodacom tunaamini kuwa vijana wanaweza kuleta mapinduzi makubwa katika sekta mbalimbali iwapo watawezeshwa,hivyo tunadhamini mashindano haya tukiamini kuwa vijana wenye vipaji wanaoshiriki wataweza kujitangaza na kujulikana ambapo katika siku za usoni ni rahisi kujiajiri kupitia katika sanaa”Anasema Nkurlu.
Pia alitoa wito kwa wakazi wa jijini Dar es Salaam kujitokeza kwa wingi katika shindano hilo ili kuwapa moyo vijana watakaotoa burudani kali pia na kuweza kununua bidhaa mbalimbali za Vodacom zitakazopatikana kwa bei nafuu kabisa kiwanjani hapo kama vile Modem na Simu aina ya Samsung E1205 zote zikiuzwa kwa shilingi 25,000 tu”Alisisitiza Nkurlu.
Share on Google Plus

About ahmed

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment